Misikiti ya Shia na Husseiniyah (ukumbi wa kidini) katika maeneo tofauti huko Tanzania huandaa maombolezo ya Muharram ya kuadhimisha mwaka wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS).
Kwa mujibu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania, Mashia wenyeji na wanachama wa jumuiya ya Khoja Shia Ithna Asharia wakishiriki katika maombolezo hayo ya kukumbuka kuuawa shahidi Imamu Husein (AS).
Mipango hiyo ni pamoja na ukariri na hotuba katika lugha tatu, yaani Kiingereza, Kiswahili na Kiurdu.
Kundi la Khoja Shia Ithna Asharia Jumapili lilipandisha bendera ya maombolezo ya Muharram na kuzindua mfano wa Vita vya Karbala jijini Dar es Salaam.